FOOTBALL FOR GOOD HEALTH AND RECREATION
Silver Pipe Veterans ni kikosi cha timu ya mpira wa miguu chenye makazi yake jijini Dar es Salaam - Tanzania, kiundwacho na vijana na wazee wa makamo. Muunganiko huu unakutanisha rika tofauti, wenye taaluma mbalimbali kwa lengo kuu hasa ikiwa ni kujumuika kwa mazoezi ya viungo, kucheza mpira wa miguu kwa manufaa ya ki-afya na kufurahi pamoja. Pia mjumiko huu, umeundwa kwa dhumuni la kusaidia shughuli mbali mbali za kijamii na hata kusaidiana baina yao katika nyanja mbali mbali.